Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lil Wayne kuhusu Ciara kuvaa kama ‘Weezy Mwanamke’ Halloween 2023

Ciara Iuo Lil Wayne kuhusu Ciara kuvaa kama ‘Weezy Mwanamke’ Halloween 2023

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lil Wayne amegonga muhuri wake wa kumuidhinisha Ciara kuvaa kama “Female Weezy” kwenye sherehe za Halloween mwaka huu.

CiCi alionyesha tumbo lake kubwa lenye mimba ya mtoto wake anaemtarajia, huku akiturudisha nyuma; ambapo mwaka 2011, Nicki Minaj aliiga uvaaji wa Lil Wayne kwenye video ya Birdman “Y.U. Mad”.

Ciara alivalia suruali ya kijeshi, tai nyeupe, cheni za msalaba wa almasi na kusuka nywele ndefu za kuchekesha ili kukamilisha mwonekano wa Weezy wenye tattoo za usoni na kila kitu. Pia alitupia kofia ya manyoya ya pinki ambayo Lil Wayne aliwahi kuonekana kuivaa kwenye video yake mwenyewe.

“Mimi ndiye Weezy Mwanamke,” ilisomeka Caption kwenye post zake kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumanne (Oktoba 31). “Yung Mula Baby.”

Lil Wayne alionekana kulizingatia vazi la CiCi lililomfanya aonekana kama yeye. Jumatano (Novemba 1), Lil Wayne alionyesha upendo kwa mwimbaji huyo wa “Goodies” kwenye Twitter kwa kuandika, “Ci Ci umeua!!!!!!! I fkn luv it,” Weezy aliandika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live