Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lil Wayne kortini kwa kutishia kumtwanga risasi mlinzi wake

Lil Wayneeee.jpeg Lil Wayne aburuzwa kortini na mlinzi wake kwa kumtishia kumtwanga risasi

Sun, 3 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa Lil Wayne ameburuzwa Mahakamani na mlinzi wake wa zamani Carlos Christian ambaye amemshtaki kwa kumtishia kumpiga risasi na kumpiga ngumi ya sikio.

Kwa mujibu wa TMZ Carlos Christian aliwaambia polisi kuwa Lil Wayne alifanya tukio hilo hilo Disemba 2021 nyumbani kwake Hidden Hills, California wakati wakiwa kwenye mzozo.

Nyaraka za mahakama zinadai Carlos aliingia gharama za matibabu, alipoteza mshahara na alipatwa na mfadhaiko wa kihisia kutokana na tukio hilo pia amemshtaki Lil Wayne kwa kudai fidia na adhabu.

Kwa upande wa vyanzo vya Lil Wayne vimekanusha mashtaka hayo kwa kusema rapa huyo hakuwa na silaha na tukio hilo halijawahi kutokea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live