Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lil Ommy amuomba Nape kumpa mtaa Profesa Jay

Lil Ommy Prof Jay Lil Ommy na Prof Jay

Thu, 19 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji maarufu wa Omary Tambwe 'Lil Ommy' amemuomba Waziri wa Teknolojia ya Mawasiliano, Nape Nnauye kuupa jina mtaa mmoja kwa Jina la msanii maarufu nchini, Jpseph Haule 'Prof Jay' ili kutambua mchango wake katika tasnia ya muziki nchini.

Ikumbyukwe kuwa, Prof. Jay yupo ICU akipigani uhai wake kwa miezi kadhaa sasa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na maradhi yanayomsumbua ambapo hivi karibyuni mkewe, Grace alisema anaendelea vizuri.

"My brother Professor Jay, GET WELL SOON nabakia kama mdau na mshauri na ikiwa sijui sana maswala ya kuweka majina ya Watu Maarufu kwenye Mitaa ila kwa heshima ya Prof Jay nahisi anaweza kuipata heshima hii.

"Kwenye zoezi linaloendelea la Anuani za Makazi, Kaka yetu, Mhe Waziri, Nape Nnauye kama itapendeza na protocol zikiruhusi basi our brother Professor Jay afikiriwe kwenye hili. Kama unaunga mkono Comment #MtaaWaProfJay.

"Nitajie Ngoma zako 5 kali za Prof Jay. Wiki hii nitatoa Special Playlist ya Nyimbo 50 au 100 za Professor Jay. Nitakwambia inapatikana wapi (Faida yote ya Playlist kimapato inaenda kwake direct kwa wasimamizi wa kazi zake)," amesema Lil Ommy.

Naendelea kumuombea my brother @ProfessorJayTz apone na arudi ktk hali yake ya kawaid. He is an ICON, Inspiration and most of all, a Game Changer! Kama itapendeza Mhe Waziri, Kaka @Nnauye_Nape tumfikirie Prof Jay kumpa jina la Mtaa! AMEIPIGANIA SANA SAA.

"Viwango vya heshima ya watu waliofanikio ni Kubwa sana kuliko wale ambao bado! Utii wao, Unyenyekevu wao ni hali ya juu sana! Be humble!," amesema Ommy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live