Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lil Durk: Sipendi 'masnich'

Lil Durk.jpeg Lil Durk

Thu, 25 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa Lil Durk a.k.a The Voice kutoka pande za Chicago ameweka wazi sababu kubwa iliyosababisha awachukie masnitch kwenye maisha yake.

Kwenye interview yake ya jana usiku na Dj Akademiks kupitia podcast yake ya 'Off the record', Lil Durk alielezea ni jisni gani baba yake alipoteza maisha kutokana na madhara ya kusalitiwa na rafiki yake ambaye alimchoma baba yake Lil Durk kwa watu waliokua wakimtafuta na mwisho wa siku akajikuta amebakiwa na mzazi mmoja mama yake mzazi.

Wakati akielezea ni kwanini hawapendi marafiki wenye tabia ya usaliti (masnitch) Lil durk aliahidi kuwapunguza wasanii wote wenye tuhuma za usaliti na kuahidi kutoshirikiana nao kwenye kazi yoyote kwenye maisha yake.

Lil Durk anafanya vizuri sana sasahivi na wimbo wake mpya unaitwa All my life kamshirikisha rapa J cole, All my Life ni ngoma ya kwanza kutoka kwenye albamu yake mpya ya nane “ALMOST HEALED” inayotarajiwa kutoka tarehe 26 mwezi huu Kwa stori zaidi ya Lil Durk na zingine za unyamwezini hakikisha unasikiliza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live