Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lifahamu kundi jipya liloahidi kuupeleka muziki wa bendi levels za kimataifa

Screen Shot 2020 08 11 At 4.52.35 PM 660x400.png Lifahamu kundi jipya liloahidi kuupeleka muziki wa bendi levels za kimataifa

Tue, 11 Aug 2020 Chanzo: millardayo.com

Najua Nina watu wangu wanaopenda burudani hususani kupitia muziki wa live sasa nina habari njema ninayotaka kukujuza ni kwamba kuna vijana zaidi ya saba wenye utashi mkubwa ambapo wameungana kwa pamoja ili kuhakikisha Muziki wa bendi ufike mbali kimataifa

Kundi hilo liitwalo  Str8uplive linaundwa na wakali wakiwemo Zungu The Drummer, Danny Fingers, T Bway, Dj Skadi, Dj Ally, Dj Joozey, Dj Bike, Dj Skit na wengineo.

Akizungumza na Millardayo.com & Ayo TV mmiliki wa bendi hiyo alisema ‘Kundi hili lina miezi kadhaa tangu limeanzishwa na mpaka sasa tumeshafika Mwanza, Arusha pia hapa Dar es Salaam tuliweza kuonesha uwezo wetu na utofauti wetu na bendi zingine ni kwamba muziki unaopigwa wowote na vijana hawa wanatumia Ala za Muziki kuonesha uwezo walionao’– Sniper Mantana

‘Lengo letu ni kutaka nchi yetu inapata heshima kupitia muziki wa bendi naamini kuna siku watu wataamini ninachosema haijawahi kutokea hiki kinachofanywa na hao vijana ambao kila mmoja ana uwezo wake wa kitofauti’- Sniper Mantana

‘Mpaka sasa tumeshafanya shows Mikoa ikiwemo Arusha, Mwanza, Dar es Salaam na mapokezi si ya kitoto na vile tunavyotarajia kiukweli tunawashukuru mikoa hiyo tuliyopita na kuhusu mikoa  mingine wakae karibu na mitandao yetu ya kijamii  Str8uplive ambapo tutakuwa tukiwapa habari mbalimbali’- Sniper Mantana

.

.

.

.

.

.

.

Chanzo: millardayo.com