Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Lifahamu Gereza la kifo nchini Libya

Abu Salim Dehghanpisheh Ybqmih Lifahamu Gereza la kifo nchini Libya

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mnamo mwaka wa 2011 kupatikana kwa kile kilichoaminika kuwa kaburi la pamoja la zaidi ya wafungwa 1,200 waliouawa katika jela ya Tripoli ya Abu Salim mnamo 1996 kuliibua kumbukumbu zenye uchungu kwa wale ambao walisubiri miaka kufahamu hatima za wapendwa wao.

Kaburi hilo lilifungua majonzi ya wnegi kuhusu hali ilivyokuwa katika gereza hilo .

Baadhi ya vipande vya mifupa ya watu vilipatikana vimetapakaa katika maeneo kadhaa.

Eneo hilo ndilo maafisa wanadhani wafungwa wengine 1,270 walizikwa baada ya kile kinachojulikana kama mauaji ya Abu Salim, mojawapo ya visa vya kutisha kabisa vya utawala wa Kanali Gaddafi.

Chini ya utawala wa Gaddafi, Abu Salim mara nyingi ilikuwa ndio makao ya wafungwa wa kisiasa, wanaodaiwa kuwa itikadi kali za kidini na wapinzai wake.

Familia za wahanga wa 1996 kwa muda mrefu walikuwa wakingoja majibu na siku hiyo walikumbana na kile walichohofia sana -kwamba jamaa zao waliokuwa wamekamatwa waliuawa .

Mtu mmoja aliyekuwa msaidizi wa Gadhafi aliyezuiliwa baada ya kuporomoka kwa utawala wake alidai kwamba maiti zilitupwa ndani ya shimo lililochimbwa ndani ya eneo la gereza. Alisema tindikali /asidi ilimwagwa juu ya shimo kisha lingefunikwa kwa lami .

Ilichukua karibu miaka kumi kabla ya utawala wa Gadhafi kukiri hadharani kwamba mauaji yalifanyika katika gereza hilo. Wakati wote huo, familia za wafu ziliendelea kupeleka chakula kwa wapendwa wao ambao waliamini kuwa wako hai.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live