Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Licha ya kuzawadiwa gari, haijazuia S2Kizzy kufuta nyimbo za Rayvanny YouTube

TETEMA RAYVANNY S2KIZZY Licha ya kuzawadiwa gari, haijazuia S2Kizzy kufuta nyimbo za Rayvanny YouTube

Mon, 29 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kitendo kushushwa nyimbo za ‘Tetema’ ambayo Rayvanny amemshirikisha Diamond Platnumz na ile ya ‘Mama Tetema’ ya Maluma Ft Rayvanny kwenye mtandao wa YouTube kimewaudhi wengi huku wakimtaja producer S2Kizzy kuwa ni mtu mwenye kinyongo na Rayvanny, na kinacho waumiza akili watu, ni kwanini anayafanya yote haya baada ya Rayvanny kuondoka WCB.

Maei 10, 2019 Rayvanny alimzawadia gari producer S2Kizzy aina ya Mark X kama zawadi yake ya birthday ambapo producer huyo husherehekea siku yake ya kuzaliwa kila ifikapo Mei 10 ya kila mwaka.

Akiwa kwenye kipindi cha Block 89 cha Wasafi Fm, S2Kizzy alifanyiwa surprise na Rayvanny akiwa na ufunguo wa gari.

Kikubwa Rayvvany alidai amefanya hivyo kama sehemu ya kushukuru mchango wa producer huyo kwa kumtengenezea ngoma nyingi ambazo zimekuwa ni pendwa, ikiwemo Mama Tetema ambayo ilikuwa na miezi mitatu tu, toka itoke Februari 7, 2019.

Kingine kilicho msukuma zaidi Rayvanny kufanya hivyo, ni baada ya kuona S2Kizzy anasumbuka kuhusu usafiri, muda mwingine kupanda bajaji anapowahi studio sessions.

S2Kizzy ambaye alimwaga chozi la furaha hadharani, aliahidi kuwa ndugu wa Rayvanny maisha yake yote, ikumbukwe gari ilikuwa nje na mikataba yao ya kufanya kazi kama producer na msanii.

Ni kweli ndugu hugombana, ila kwa hili, linazua picha kubwa na mbaya kati ya hawa wawili, japo hakuna hata mmoja kati yao amewahi liongea kwa kina hili, mbali na S2Kizzy kukana kuwa sio yeye, japo jina lake kwenye claims linaonekana kama Salimin Kassim.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live