Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lesa wa Planet Bongo aondoka East Africa Radio

Lesa Wa Planet Bongo Dgv Lesa wa Planet Bongo.

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa kipindi maarufu cha burudani nchini, Planet Bongo kinachoruka East Africa Radio, Lesa ametangaza kuondoka katika kituo hicho baada ya kukitumikia kwa miaka mitano.

Ndani ya East Africa Radio Lesa alikuwa anaongoza show ya Planet Bongo kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, pamoja na Bongofleva Top 20 kila Jumamosi.

Jana Aprili 12, 2024, Lesa kupitia ukurasa wake wa Instagram alitangaza kuondoka redio hiyo na kuwashukuru kwa kumpa nafasi ya kujifunza na kusisitiza bado wataendelea kuwa familia yake.

“Such a wonderful journey, 5 years nimekuwa hapa kujifunza na kukua ndio kitu ambacho, asante sana East Africa [Radio/TV].” aliandika Lesa na kuongeza. “Ni kwaheri ila si ya kuonana maana sisi sio milima tutakutana marafiki na familia nilioipata hapo, ni kumbukumbu nzuri kwa popote nitakapokuwa.” alisema Lesa.

Kwa sasa Planet Bongo inayosikika kuanzia saa 01:00 mchana hadi 04:00 jioni, imebaki chini ya Rich Msafi na Piwa Magic ambaye alichukua nafasi ya Dullah Planet.

Mrembo huyu anakuwa Mtangazaji wa nne kuondoka katika show ya Planet Bongo ya East Africa Radio baada ya JR Junior, Frida Amani na Dullah Planet.

Utakumbuka JR Junior kwa sasa yupo Times FM, Frida Amani ambaye anafanya muziki pia alijiunga na Clouds FM na Dullah aliyejiunga na Crown FM ya Staa wa Bongofleva, Alikiba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live