Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Legacy ya Daz Nundaz ni Soulful

Daz Nundaz Daz Nundaz.

Mon, 29 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nikupe mchongo. Kama unapeleka maombi ya kazi taasisi yoyote, ongeza kwenye CV yako, kipengele kuwa ulihudhuria induction ceremony ya Daz Nundaz, Julai 19, 2024, Warehouse Arena, Oysterbay.

Nakuhakikishia, bosi wako ajaye alikuwepo Warehouse na alichenguka vibaya. Aliimba nyimbo za Nundaz mwanzo mwisho. Hivyo, CV yako ikionesha ulishuhudia moto wa Nundaz Warehouse, atakuona resourceful. Atakuajiri.

Tuanze na audience. Mabosi walijaa. Waligombea tiketi za VVIP na VIP. Waliolipa regular walirudi getini kuomba ku-upgrade tickets. Hiyo ni nguvu ya Bongo Flava ambayo inatunzwa na Bongo Flava Honors.

Pili, Bongo Flava Honors ilifanya kilichoonekana hakiwezekani, kikawezekana. “Daz Nundaz kufanya kazi pamoja tena, abadan!” walisema wadau. Governing committee ya Bongo Flava Honors ikasema inawezekana. Maarifa kidogo, bila miguvu, Nundaz wakarudi pamoja. Halafu imara.

Tatu, performance ya Nundaz. Mtu nne, Ferooz, Daz Baba, La’Rhumba na Sajo wakiwa na Swahili Blues Band, walifanya maajabu ya takriban dakika 150. Sauti zenye nguvu juu ya ala zilizonyongwa live kwenye orchestra. Walivyoachiana nafasi jukwaani na walivyopokezana. Nundaz ni professionals.

Ilikuwa event ya kuwaheshimisha Nundaz. Kila kitu kilifanyika kuwapa heshima yao. The host, Sugu The Jongwe, alifanikisha kila kitu, akakabidhi plaques kwa members wote wa Nundaz. Hata Mtumishi wa Mungu, Noely Kapinga a.k.a Critic, hakukosa yake.

Ajabu, ikageuka karaoke night, wimbo kwa wimbo, audience haikuacha Nundaz waimbe peke yao. It’s mass karaoke. Hapo ikadhihirisha legacy ya Nundaz kupitia nyimbo zao ni soulful. Nundaz wapo ndani mno ya Watanzania kwa rekodi zao zisizosahaulika.

Barua iliimbwa na kila mtu, neno kwa neno. Kamanda, audience ili-sing along mstari kwa mstari. Maji ya Shingo, Starehe, Namba 8, Wife, Jahazi, Shuka Rhymes, Nitafanya Nini, Kioo, Matatizo, Elimu Dunia, Ndege Mtini, haisahauliki ukumbi ulivyo-bust kelele, ilipopogwa Jirushe, kisha Nipe Tano ilifunga kazi kibingwa.

Ungeona raha Ferooz alivyobeba leadership. Unge-enjoy character ya Daz Baba, ungependa swaggers za La’Rhumba, michano ya Sajo ilikuwa mwake. Hey Nundaz, we need some more!

Ndimi Luqman MALOTO

Chanzo: www.tanzaniaweb.live