Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lebron James ajibiwa na Squid Game

Squid.jpeg Lebron James ajibiwa na Squid Game

Wed, 27 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wiki mbili zilizopita mcheza kikapu wa timu ya Lakers, Lebron James alifunguka kwamba hajapenda series ya Squid Game jinsi inavyoisha mwishoni, wakati anapiga story na mchezaji mwenzake Anthony Davis.

Lebron alikuwa anaongea na vyombo vya habari baada ya mechi ya Lakers na Golden State Warriors. Wakati anaondoka Anthony Davis alimfuata na kumuuliza kama ameitazama Squid Game, na Lebron alimjibu “Yeah, I did not like the ending though. I know they start it off with a season 2”.

Kauli hiyo ya Lebron James imejibiwa na muandishi na director wa Squid Game, Hwang Dong-Hyuk ambae alisota kwa miaka 10 kutafuta kampuni ya kufanya nayo kazi.

“Ushawahi kuitazama Space Jam 2?” jibu la kwanza la Hwang wakati anaongea na muandishi wa The Guardian kuhusiana na Lebron kuikosoa story yake mwishoni.

“Lebron ni mtu poa na anaweza kuongea lolote analotaka, namuheshimu. Nashukuru sana ametazama series yote, lakini sitaweza kubadilisha mwishoni ilivyoisha. Huo ndio mwisho wangu nilivyopanga iishe. Kama yeye ana idea ya mwishoni jinsi ingeisha sawa anaweza kutengeneza ya kwake”

Hwang hakuishia hapo alimalizia na kusema “Akitengeneza ya kwake nitamtafuta na kumtumia ujumbe, nimependa show nzima kasoro mwishoni”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live