Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lava Lava: Nilinunua viatu kwa tsh milioni 4 bila kujua

Lava Lava Shukrani Lava Lava

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii Lavalava amesema kwenye upande wa mavazi kitu pekee alichowahi kununua kwa gharama kubwa ni kiatu ambacho alikinunua kwa thamani ya shilingi milioni nne kwa shinikizo la mchumba wake wa kizungu.

"Kuna siku mchumba wangu ni mzungu yuko kwao Ulaya alinipigia simu akaniambia yupo kwenye mall moja ameona kiatu kizuri nimuongezee pesa aninunulie, thamani yake ni kama dola 2,000 hivi au 1,500 (zaidi ya Tsh milioni 4).

"Nikaamua kumtumia namba yangu ya kadi ya benki ili aswap alipe hiyo pesa, bahati mbaya akajikuta amelipia pesa yote pasipo kuongezea kiasi chake alichokuwanacho.

"Aaaaaah niliumia sana kuona pesa yangu imekatwa sababu ya kiatu ila ingekuwa mimi kwa akili yangu nisingenunua," alisema Lava Lava.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live