Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lady Jaydee anena "hiyo kauli na iishe rasmi"

Jide 660x400.jpeg Lady Jaydee anena "hiyo kauli na iishe rasmi"

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: millardayo.com

Habari ya Tanzania kupata Rais wa kwanza Mwanamke ambae ni Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ndio inayo-trend hadi sasa na Watu mbalimbali maarufu hawajasita kutoa maoni yao akiwemo Mwimbaji wa siku nyingi wa Bongofleva Lady Jaydee.

Baada ya Rais Samia kupokea Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali Charles Kichere Ikulu Chamwino Dodoma jana, Jaydee aliingia kwenye ukurasa wake wa twitter na kuandika maneno haya ikiwa ni baada ya Rais Samia kutoa maelekezo ya kupelekewa Ripoti ya pesa zilizotumika kuanzia January 2021 na pia kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania.

Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu jana.

Jide aliandika “Ile kauli ya huo ni umama na iishe rasmi, asanteni” ……Jide aliandika maneno haya kwenye Twitter ambako Watu mbalimbali pia walimimina kauli za pongezi kwenye moja ya hotuba zake za kwanza kabisa toka Rais Samia Suluhu aapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Inawezekana Jide kama walivyo wengine wanafikisha ujumbe kwamba hata Wanawake wanaweza hivyo sio wa kuchukuliwa legelege.



ULIPITWA? TAZAMA HAPA CHINI RAIS SAMIA ALIVYOHUTUBIA NA KUTANGAZA KUMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA MAMLAKA YA BANDARI..
Chanzo: millardayo.com