Kabla ya Yahaya, Jaydee aliachia atomic “Joto Hasira” aliomshirikisha Profesa Jay. Halisahauliki lile sokomoko la baada ya Joto Hasira. Jide aliufanya uwanja wa mapambano uwe tambarare dhidi ya most powerful men kwenye mzingo wa burudani Bongoland. Jide ni fighter. Ni tafsiri ya super-confident lady.
Kila mtu anafahamu Jaydee ni bold, ni fearless. Hata hivyo, mapenzi yalimpelekesha akawa “Teja”. Afrika Mashariki ikaimba “Teja wa mapenzi”. Na hii inajenga wasifu mpana wa Jide kimuziki. Anaweza kuandika, kutunga na kuimba kila kitu. Wimbo kwa wimbo, albamu hadi albamu, Jide haimbi tu mapenzi na mikasa ya ulimwengu, bali pia shule ya maisha.
Mkwaju “Historia”, ni elimu ya nidhamu ya pesa na maisha. Ukitembelewa na fedha, ukaleta fahari kwenye matumizi, zitakwisha, utageuka historia ukiwa bado unaishi. “Msimwone jamaa vile, alikuwa na pesa yule!” Ni kazi ndani ya albamu ya sita ya Jide, “Nothing But The Truth”, mwaka 2013.
Kuna bomu “Ndindindi”, lililoifanya Tanzania iwe na hekaheka kwenye mitandao mwaka 2016. Ndindindi ilisafisha njia ya albamu ya saba “Woman”, iliyofungasha hits kibao; “Nasimama”, “Sawa na Wao”, “Together”, aliofanya na Spicy kutoka Nigeria.
Ulifika mwaka 2021, dunia ilipoanza kujinasua kwenye utumwa wa balaa gonjwa Covid-19, Lady Jaydee aliona ulikuwa wakati mwafaka wa kuikabidhi dunia albamu ya nane. Akaiita “20”. Ni santuri double CD level. Nyimbo 20 kamili ndani yake.
Maajabu ya Lady Jaydee kama kawaida. “I Miss You” was a trendy song. “Good Vibes” was the most streamed. Maisha ni matamu sana kama ukichagua kujipenda mwenyewe, ndiyo maana “I Love Myself” ni smash ndani ya albamu ya Jide “20”. Ukitaka best-loved chorus ambazo Jide amepata kushirikishwa, utazipata ndani ya mkwaju “Chorus”.
Jaydee alifanya chartbuster song “Kupendwa Raha”, aliomshirikisha the chartbuster artist, Mr Blue. The love appealing song “Don’t Go” with Niniola kutoka Nigeria is one of the most played. “Harusi” aliofanya na Mandojo na Domokaya, ni goma la kikwetukwetu.