Jina Bongo Flava halikuwa verified. Muziki ulionekana ndoto kuwa industry. Y2K iliambatana na sauti ya kike. Wimbo “Nakupenda” ulimtambulisha bidada newcomer kwenye game mwaka 2000.
Single hiyo imo kwenye compilation album “Asubuhi ya 2000”. Sauti ya bidada ikapendezesha hook ya ngoma “Mambo ya Fedha”, mali ya big dawg, Sugu “Mr II”. Hakuna aliyetabiri haraka kuwa angekuwa kiranja wa kike wa Bongo Flava.
Mpate katika masafa ya Lady Jaydee. Ukimsaka kwa frequency za Binti Komando pia anasomeka. Kuna kipindi alipenda kujiliza, akajiita Binti Machozi. Siku hizi hapendi hilo jina. Chaneli ya Mama Somefood ni pay-to-eat Nyumbani Lounge. Utambulisho wa passport ni Judith Wambura Mbibo.
Kasi ya kuandika na kutengeneza muziki, ni nuru ya Jaydee kuhusu mahali alipokuwa anakwenda. Sequential hits nonstop; “Ne-Syum Problema”, halafu legendary ballads, “Mpenzi Wangu” featuring pioneer D-Rob from Kwanza Unit, kisha “Sema Unachotaka” aliofanya na grand OG, Terry Fanani kutoka Hard Blasterz Crew.
Reverse your calendar. Tupo mwaka 2001. Jaydee a.k.a Jide, anaiweka nchi kwenye standstill kupitia jam “Machozi”. Ile sauti akiimba “nailazimisha furaha, lakini moyoni nina majonzi”, ikaongopea wengi waliodhani Jide ni “cha-kudeka”. Battle za kimaisha zilimpambanua kuwa ni street-tough lady, Komando, Anaconda.
Albamu ya “Machozi”, ni moja ya santuri zilizothibitisha muziki wa Kiswahili ni kitalu cha ngawira. Mawe “Waweza Kwenda”, “Penzi la Milele”, “Umuhimu Wako” collabo na Sir Nature, na nyingine, ziliifanya Machozi kuwa albamu ya thamani kubwa sokoni.
Sogea mwaka 2003, Jide anatoa albamu “Binti”. Ndani yake, alifanya kila kitu kumhamasisha mtoto wa kike, kujitambua. Halafu, aliwapa sana za chembe wanaume.
Jaydee aliifanya issue ya majanki kulelewa na mashangazi kuwa kesi endelevu. Akaingia booth na MwanaFA, akatoa kitu “Wanaume Kama Mabinti”, akaona dawa haijakolea, akarudi booth na Papii Kocha, wakaifanza remix.
Oktoba 25, 2024, Lady Jaydee atapokea hall of fame plaque ya Bongo Flava Honors. Warehouse Arena, Oysterbay ndiyo spot. Tuna-preview greatness ya Jide; the undeniably Mom-In-Chief wa Bongo Flava.
Ndimi Luqman MALOTO