Laana ya Kanumba ndiyo inamtesa Wema Sepetu? Hi ni kama swali ambalo ndani yake kuna funzo kubwa hasa katika masuala ya afya ya uzazi.
Uhusiano na aliyekuwa nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba ndiyo uliyomfungulia Wema milango katika tasnia ya filamu.
Kanumba fundi hasa wa kuigiza ndiye alimuambia anaweza kuigiza na kumpa nafasi katika filamu, 'A Point of No Return'.
Hata hivyo, kupitia App yake Wema anadai katika uhusiano wao alitoa mimba mbili za Kanumba kitu ambacho anajutia hadi leo na anaona imekuwa kama laana kwake kutokana na kutopata mtoto hadi sasa.
Kwa miaka mingi sasa, Wema amekuwa akipambana kutafuta kuzaa mtoto wa kumpa faraja lakini mambo yamekuwa magumu kwani mpaka sasa jambo hilo ni kama limekuwa kitendawili kwake.
Mwenyewe anasema ameshatumia kila aina ya dawa kujaribu kupata mtoto, sio za mitishamba wala za hospitali, hapa ndipo utagundua kwamba Mungu ndiye mpaji pekee.
Je, ni kweli laana ya Kanumba inamtafuna Wema?