Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Kyle Walker aiomba radhi familia kisa kumwanika mchepuko wake

Kyle Walker X Annie Kyle Walker aomba radhi kisa kumwanika mchepuko wake

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Manchester City, Kyle Walker, ameiomba radhi familia yake kwa “kufanya uamuzi wa kipumbavu” kufuatia wiki kadhaa za tetesi kuhusu maisha yake binafsi.

Mchezaji huyo ameliambia gazeti la the Sun, kuhusu uhusiano wa kimapenzi [mchepuko] na Lauryn Goodman, mtangazaji wa TV.

“Nilichokifanya ni kibaya mno,” alisema, huku akimuomba radhi mke wake, Annie Kilner, ambaye ni mja mzito, na ambaye tayari wana watoto watatu pamoja.

Walker, 33, ameliambia gazeti hilo: “Nilichokifanya ni kibaya, na nabeba lawama zote.

“Nilifanya uamuzi mbaya. Siwezi hata kufikiria kile Annie anachokipitia kwa sasa. Nimejaribu kumuuliza, lakini ni maumivu tu.”

Akizungumza kwa matarajio ya kupata faragha kwenye familia yake, Walker alisema: “Matendo yangu yamesababisha maumivu makubwa kwa watu wengi. Naomba radhi kwa sababu kama mtu wa familia, hili halitakiwi kutokea.”

The Sun limeripoti kuwa Walker alipata watoto wawili na Bi Goodman, wakati akiwa kwenye ndoa na mkewe Annie.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live