Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwisa: Promo kubwa lakini D Voice hana uwezo

Diamond D Voice Kwisa: D Voice hana uwezo

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji na mdau wa masuala ya burudani, Kwisa Thompson maarufu kama Kwisa Kamanda Mzee Mkavu amedai kuwa, msanii mpya aliyesainiwa na Diamond Platnumz katika Lebo yake ya WCB, D Voice hana uwezo kama ambavyo watu wanadhani.

Kwisa amesema kuwa, nyimbo za msanii huyo zinazofanya vizuri ni zile tu ambazo amewashirikisha wasanii wakubwa wa WCB lakini nyimbo alizofanya yeye peke yake wala hazijulikani, hiyo inaonesha kuwa uwezo wake bado ni mdogo sana.

"Promotion ya D Voice imekuwa kubwa kuliko uwezo wa msanii mwenyewe, yeye ndiye msanii pekee aliyetambulishwa kwa ukubwa kuliko wasanii wote waliowahi kujiunga wasafi.

"Lakini kwa jinsi alivyotumbuiza siku ya utambulisho na ikiwa hatajiongeza basi hamna kitu. Ukiangalia nyimbo zake zinazofanya vizuri sasa hivi ni zile alizowashirikisha kina Zuchu, Mbosso, Lavalava na Diamond Platnumz.

"Lakini hakuna wimbo alioimba peke yake unaofanya vizuri hii inaonyesha bado hana uwezo na hata hizo nyimbo zinafanya vizuri kwa sababu ya hao wasanii wengine sio yeye. Tumpe muda labda atafanya vizuri huko mbeleni sasa hivi bado ni mapema sana," amesema Kwisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live