Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kweli Zuchu alikuwa bize kushindwa kuhudhuria harusi ya Nandy?

ZUCHU NANDYYY Kweli Zuchu alikuwa bize kushindwa kuhudhuria harusi ya Nandy?

Tue, 16 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii kutoka WCB, Zuchu ni miongoni mwa Waalikwa katika Ndoa ya Nandy pale Mlimani City lakini hakuweza kutokea katika Event hiyo, haikuwa gafla, alimwambia Nandy Mapema kwamba Hatoweza Kutokea katika Event hiyo Maana ana mambo mengine anafanya.

Hata hivyo baada ya ndoa ya Nandy, Zuchu aliwasiliana na Nandy, kisha akampongeza kwa hatua kubwa aliyofanikiwa maana msanii wa kike Kuolewa sio kitu Kidogo.

Hivi ni kweli kwamba Zuchu alishindwa kutokea shughuli ya Nandy kisa yupo Busy au aligoma tu ili Kulinda Brand yake na kuendelea kuamisha watu kuwa hayupo sawa na Nandy?

Pia, tukumbuke kwamba Wasanii wa Wasafi hawaruhusiwi kuhudhuria Mishe mbalimbali zenye watu wengi maana mabosi watadai chao mapema mno.

Lakini habari njema zaidi ni kwamba Zuchu amethibitisha kwamba yupo Vizuri sana na Nandy, wanaelewana kabisa, ni Muziki tu ndio unafanya watu hawa waonekane kama wana bifu.

Lakini Ukifatilia vizuri ile voice note ya Nandy utagundua kabisa, watu hawa wanashindwa tu kuweka wazi mambo, ni wanafiki tu, hakuna cha ushikaji wala nini, wanachukiana sana hawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live