Kipande cha video alichokiachia Francis Cesar maarufu kama Majizzo, ambaye ni CEO wa EFM na TVE, akimtangaza mchekeshaji Emmanuel Mgaya naarufu kama Masanja Mkandamizaji kama mtangazaji mpya wa chombo hicho cha habari umezua gumzo.
Hii inakuja baada ya watangazi wake Maulid Kitenge na Gerald Hando kuondoka na kwenda Wasafi FM huku B Dozen na Oscar Oscar ikiwa haijulikani wanaelekea chombo kipi cha habari.
Majizzo ameandika Haya:
Kifaa cha kipekee kilichosaidia uvumbuzi wa mengi, kifaa chenye matumizi ya thamani kubwa lakini kimetengezwa katika saizi tofauti kiweze kumilikiwa na wengi.
Maisha yangu yemekuwa hivyo, nimekuwa nikimuomba Mungu niweze kuona mbali kama #Telscope, lakini nisiwe mwenye kujikweza ili Watanzania wenzangu wa kawaida kabisa, wale wa kule uswahilini na kwingine kugumu nilikotoka wajue mimi ni mwenzao. Asante Mungu, imeendelea kuwa hivyo.
#Telescope: Miaka 9 iliyopita tuliona thamani kwa Watangazaji, thamani ambayo kwa wengine ilipuuzwa sana. Tukakuza majina yao na kuyalinda, na sasa nina furaha sana kwamba thamani niliyotamani waipate wanaipata.
#Telescope: Muda umefika, redio zinahitaji ladha mpya, tunahitaji kutoa nafasi kwa vijana wapya, hatuwezi kuwa na sauti zilezile kila mahali.
Kama ambavyo nimeongea mara nyingi, mimi nitatoa nafasi kwa vijana wapya. Lakini mtakubaliana nami kuwa hii ni biashara na inahusisha mchakato kama vitu vingine, lazima tuanzie mahali twende kwa hatua nzuri.
#Telescope: Tuanze na watu ambao tunawajua, lakini hatujui upande wa pili wa vipaji vyao. Masanja tunamjua kama mchekeshaji na kwenye ‘media’ yuko upande wa mahubiri tu. Hatujamuona akisoma magazeti.
#Telescope: Kama ambavyo tulitambulisha mtindo mpya wa kusoma magazeti ambao hivi sasa unaigwa sehemu nyingi, leo tunatambulisha msomaji mpya wa magazeti katika namna ya kuvutia. Namleta kwenu @mkandamizaji.