Beyonce Na Solange Knowles Wana Half Brother wao Nixon ambaye hawajawahi Kukutana Nae, Pamoja Na Kwamba Wanaishi sio mbali Nae.
Mwaka 2007 Baba Mzazi Wa Beyonce Alikutana Kwa Mara Ya Kwanza Na Muigizaji Kutoka Canada Alexander Wright, Mzee Huyo Kidume Akatupia Ndoano Yake, Na Mwanzoni Alexander Alimkatalia.
Ila Mzee Alikuwa Yupo Serious, Akamwambia Hatoondoka Mpaka Amkubalie Kutoka Nae Out, Baada Ya Siku Kadhaa Alexander Akakubali Kutoka Out.
Kipindi Anakubali Kutoka Out Na Matthew Knowles Baba Yao Kina Beyonce Na Solange, Mzee Huyo Alikuwa Bado Yupo Katika Ndoa Na Hapo Aliamua Kuchepuka.
Kuchepuka Huko Kukai Cost Ndoa Yake Na Mama Beyonce Tina Knowles Na Maza Huyo Akaomba Talaka 2009 ... Lakini Sio Tu Kuchepuka Huko Kuliigharimu Ndoa Yake, Lakini Pia Baba Huyo Aligharimu Mahusiano Na Watoto Wake, Kwanza Beyonce Alimpiga Chini Kama Manager Wake, Ila Pia Kiujumla Mawasiliano Kati Yao Yakapotea.
Alexander Akanasa Ujauzito Na Kupata Mtoto Wa Kiume Nixon, Na Matthew Akataka Vipimo Vya DNA Kuwa Na Uhakika Kama Nixon Ni Mwanae Na Vipimo Vikaonyesha Yeye Ni Baba Mzazi Wa Nixon.
Kupigwa Na Chini As Manager, Ikatingisha Kipato Cha Baba Yao, Na Kuna Muda Akashindwa Kabisa Kutoa Matunzo Ya Nixon, Alexander Na Mwanae Wakapitia Kipindi Kigumu Mpaka Kufikia Kuishi Katika "Mobile House" Kwa Muda Mpaka Rafiki Wa Alexander Muigizaji Mwenzake Shar Jackson Kuamua Kuwakaribisha Na Kuishi Nao Nyumbani Kwake.
Mama yake Nixon, Anajiuliza Kwa Nini Beyonce Hampendi Mdogo Wake Na Hayo Ameyasema Katika Interview Aliyofanya, Watu Wengi Wamemtetea Beyonce Kuwa Yeye Hana Ulazima Wowote Wa Kuwa Karibu Na Nixon, Wengine WanAsema Alexander Anatafuta "Kiki" Kwa Nini Amtaje Tu Beyonce Na Asimtaje Na Solange.
Alexander Anasema Kuna Muda Anakaa Na Kulia Bafuni, Mwanae Anapomuuliza Kwa Nini "Hawampendi" Lakini Pia Ukiacha Beyonce, Solange Mtoto Huyo Pia Hajawahi Kukutana Na Baba Yake
Kwa Sasa Nixon Ana Miaka 13, akitafuta Upendo Na Kujuana Na Ndugu zake.