Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa hili, Justin Bieber aamua kuachana na Muziki

Justin Bieber Aacha Muziki Mwanamuziki Justin Bieber

Wed, 29 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa muziki, Bieber anafikiria kuachana na kiwanda cha Muziki kwa ajili ya kujikita kwenye kuangalia afya yake pia ndoa yake na Hailey. Taarifa zinaripoti kwamba JB amekuwa akitaabika na msukumo ambao unatokana na kubana kwa ratiba zake.

Kwa sasa Justin Bieber ameahirisha tarehe zote zilizokuwa zimebaki kwenye ziara yake (Justice World Tour) kufuatia kugundulika kuwa na ugonjwa wa Ramsay Hunt syndrome, ambao ulimfanya apooze kwa muda upande wa kulia wa uso wake.

Chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa RadarOnline kwamba “Justin amekuwa hana furaha na mambo ya dunia kwa muda sasa, na mzigo wa umaarufu wake unamuelemea. Hata matabibu wake wamemwambia kwamba kama anachokifanya hakimpi furaha, anapaswa kufanya maamuzi magumu kukiweka pembeni.” Kilieleza chanzo hicho.

Watu wameenda ndani kabisa na kuchimbua kuwa ndio maana Justin Bieber mwezi January mwaka huu, alichukua maamuzi ya kuuza haki za Muziki wake (catalog) kwa $200M, takribani TSh. Bilioni 468 ikiwa ni miongoni mwa mipango ya kukaa mbali na masuala ya muziki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live