Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Kuzaa watoto wengi ni mtaji

Familia Kubwaa Kuzaa watoto wengi ni mtaji

Mon, 22 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika hali inayoweza kukushangaza Rais wa Urusi alitoa agizo wiki hii akiboresha tuzo inayoitwa “Mothers of Veterans”, ambayo ilianzishwa mwaka 1944 na serikali ya Umoja wa Kisovieti.

Tuzo hii inatolewa ili kuhamasisha familia kuwa na watoto wengi Zaidi, Rais Putin alisema wiki hii kwamba tuzo hiyo ambayo inaendana na zawadi ya fedha na vitu vingine vya thamani itatolewa kwa kila mama atakayejifungua watoto 10 na kuendelea.

Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kukabiliana na kupungua kwa kasi ya ongezeko la watu nchini Urusi.

Vyombo vya habari vya kimataifa, vikiwemo magazeti ya Washington Post na Express, vilitangaza habari hii kuhusu agizo hilo la rais wa Urusi, ambalo limeleta mjadala mkubwa kimataifa

Ukiachana na Urusi nchi nyingine ambazo zina idadi ndogo ya watu ikiwemo Finland ambayo inakadiriwa kuwa na watu 5,601,547.

Finland inalipa pesa za ziada kwa watu ili kupata watoto. Tangu mwaka 2013, kila mtoto aliyezaliwa katika wa mji Lestijärvi amepewa euro10,000 kupitia kwa mama yake.

Nchi nyingine ni Estonia ambayo kwa muda sasa imekuwa ikitumia pesa kuongeza idadi ya watoto wanaozaliwa, na serikali inafurahia hasa familia zenye watoto wengi zaidi. Familia ya Kiestonia yenye watoto watatu hulipwa Euro 520 kwa mwezi, jambo ambalo huwatia moyo watu ‘kupambana’ kupata watoto wengi zaidi.

Nchini Japani, idadi ya watoto wachanga wanaozaliwa imefikia kiwango cha chini kabisa katika miaka ishirini na minne iliyopita, kulingana na Business Insider.

Lakini maeneo ambayo yamepiga hatua kubwa katika idadi ya wanaojifungua ni maeneo ambayo pesa za bonasi hulipwa kwa akina mama wanaojifungua watoto wapya.

Katika mojawapo ya majiji nchini humo, yanayoitwa Ama, ambayo ni sehemu ya kisiwa cha Nakanoshima, kila mzazi anayejifungua mtoto wake wa kwanza hupewa kiasi cha yen 100,000 (sawa na dola 940).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live