Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Kutana na mwanamke anaependa kula Poda kuliko Chakula (+Video)

Mwanamke Poda Kutana na mwanamke anaependa kula Poda kuliko Chakula

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja huko New Orleans nchini Marekani aliyefahamika kwa jina la Dreka Martin, amezua gumzo mitandaoni baada ya kuweka wazi tabia yake ya kupenda kula poda (powder).

Mrembo huyo wa miaka 27 mwenye mtoto mmoja, anasema alianza kula poda miaka 10 iliyopita na kwasasa akilazimishwa kuchagua kimoja kati ya poda na msosi basi atachagua poda kwa jinsi anavyoipenda.

Anasema kwa kawaida kila siku iitwayo leo lazima ale chupa moja na hajawahi kupata matatizo yoyote ya kiafya'

Dreka anaendelea kueleza kuwa kipindi pekee alichovumilia kutokula poda ni wakati alipokuwa na ujauzito wa mwanae wa miaka 3 aitwae Faiz.

"Napenda kula poda, ladha yake ni nzuri kama inavyonukia....nimejaribu njia mbalimbali kuacha lakini nimeshindwa, kila nikiifikiria mate hunitoka. Imefika hatua kula poda naona muhimu kiasi kwamba hata siwazi kuhusu msosi"

"Niko radhi kutumia hela yangu ya mwisho kununua poda kwasababu ni kitu ninachokipenda sana."

View this post on Instagram

A post shared by ???????? ???????? (@pmtvtz)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live