Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Kutana na mwamba anayewasiliana na wanyama

Wanyama 84296 Kutana na mwamba anayewasiliana na wanyama

Sat, 12 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mohamed Abeid, mkazi wa Kijiji cha Pamba Roho kilichoko kisiwa cha Lamu nchini Kenya, huyafanya yale yanayoshabihiana na jina la kijiji chake yaani ‘kuzipamba roho’ za watu.

Abeid, mwenye umri wa miaka 46, amejaaliwa kuwa na kipawa cha kuzungumza, iwe ni kwa ishara au maneno na wanyama, na hasa punda wake.

Huenda ukashikwa na butwaa na na ukabaki na bumbuwazi, endapo siku moja utabahatika kukutana na Abeid akimwambia punda wake kwa upole; simama, kaa, nenda, rudi, hesabu moja hadi tano, cheza muziki, lia, nyamaza na kadhalika.

Cha kustaajabisha ni kwamba maelekezo ambayo Abeid anampa mnyama huyo, yote yanafuatwa ipasavyo, na tena kwa weledi mwingi utadhani anazungumza au kumwelekeza binadamu mwenzie.

Kwa mujibu wa mtandao wa Taifa Leo, ambao walifika kisiwani hapo kutaka kujua ni jinsi gani jamaa huyo kaibukia kuwa mweledi wa kuzungumza na Punda huyo, Abeid amekiri kuwa mapenzi tele kwa wanyama.

Ameasema katika kuishi kwake, katu hakumbuki kumpiga au kumdhulumu punda wake. Yeye huwazungumzia wanyama wake kwa utaratibu na heshima, ambapo humtii na kufanya yale yawapasayo.

“Kama ulivyoshuhudia hapa, nikimwambia punda ahesabu moja hadi tatu, yeye hunihesabia kwa kuudundisha ukwato wake chini mara hizo tatu. Hata nikamwamuru afanye hivyo mara ishirini, yeye huwajibika kikamilifu na kunihesabia hizo mara ishirini.

"Nikimwambia karibisha wageni kwa kulia, anafanya hivyo. Kila ninachomwelekeza yeye hufanya. Haya yote yanatokana na mapenzi ya dhati ambayo mimi huanza kuwaonyesha punda wangu tangia udogoni mwao hadi utu uzimani,” ameeleza Abeid.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live