Giovanni Vigliotto anashikilia rekodi ya Guiness ya kuwa mwanaume aliyekuwa na ndoa nyingi kuwahi kutokea duniani akiwa ameoa wanawake 105.
Ndoa zote hizo zilifanyika kati ya mwaka 1949 hadi 1981 bila talaka yoyote kutolewa.
Inaelezwa kuwa Giovanni alioa wanawake katika majimbo 27 tofauti ya Marekani na nchi nyingine 14, tena akitumia utambulisho tofauti tofauti wa uongo kila wakati.
Hakuna hata mmoja wa wake zake aliyejua kwamba Vgliotto alikuwa na wanawake wengine, kila mwanamke alijua ameolewa peke yake.
Cha kuchekesha zaidi Giovanni Vigliotto halikuwa hata jina lake halisi; bali lilikuwa jina alilolitumia wakati anaoa mke wake wa mwisho.