Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kusah asherehekea ngoma yake kufikisha watazamaji milioni 10

Kusah Mn.jpeg Kusah asherehekea ngoma yake kufikisha watazamaji milioni 10

Tue, 2 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa chipukizi wa Bongo Fleva, Kusah ameonyesha kufurahia baada ya ngoma yake ya ‘I Wish’ kufikisha watazamaji milioni 10 kwenye mtandao wa YouTube.

Kusah alisherehekea na kusema kwamba hiyo ilikuwa moja kati ya ndoto zake kuona ngoma yake inagonga watazamaji mamilioni na kumshukuru Mungu kwamba mwisho wa siku ndoto yake imetimia, miezi tisa tu tangu kuiachia video hiyo kali.

“Zilikuaga ndoto zangu za kila siku hatimae Mungu ametenda na kunifundisha kwamba kila kitu kinawezekana. Kwa upande wangu hii ni kubwa sana, milioni 10 views ndani ya miezi 9,” alisherehekea Kusah.

Kusah amesema kwamba si kila mtu aliyekuwa anamuamini katika safari yake ya kimuziki kwani wengi walikuwa wanasema hawezi kufika popote lakini hatua hii imewapiga changa la macho wale waliokuwa na dhana kama hiyo.

“Wengi walikua wakidhani kwamba huwezi kufika kokote bila kuwa chini ya Boss, Label au watu wenye nguvu kubwa haswa ila kwa sasa imekua tofauti kizuri ndio hupendwa,” alisema Kusah kwa furaha kubwa.

Vile vile, msanii huyo alichukua fursa hiyo kutoa neno na kuhimiza kwa wasanii wanaochipukia kwenye gemu la muziki na kuwaambia kwamba nafasi ni nyingi bora msanii unafanya muziki wa kuvutia

“Wadogo zangu, kaka na dada zangu ambao ndio mmeingia kwenye industry niwaambie tu kwamba nafasi ni nyingi na kila kitu kinawezekana ukiamua. Asanteni saana watu wangu,” Kusah alishukuru kwa furaha nyingi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live