Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kusah amaliza utata kwa Aunt Ezekiel

KUSAH AUNT Kusah amaliza utata kwa Aunt Ezekiel

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama unadhani zile habari za mitandaoni kwamba familia ya Kusah, haitaki kabisa kusikia habari za msanii huyo kutoka kimapenzi na Aunt Ezekiel kwa kinachoelezwa eti ni mkubwa kwake licha ya kuzaa naye mtoto, pole yako kwani mwimbaji huyo amesema wanaosema hivyo hawajui lolote juu na wawili hao.

Kusah amesema tofauti na kelele za watu, ukweli ni kwamba familia yake inampenda na kumkubali Aunt kama ambavyo yeye anavyompenda na kumkubali mzazi mwenzie huyo.

"Kitu kimoja ambacho naweza kukisema ni kwamba ukweni, Aunt Ezekiel au Mama Nono anapendwa kama ninavyompenda. Nimepitia maisha mengi, yakiwamo ya kusimangwa, ikafika muda nikaona kama nimekata tamaa, lakini kwa sasa hivi sina msongo wa mawazo kwa sababu na kipenzi changu hicho," alisema.

Kusah na Aunt wapo katika uhusiano kwa muda mrefu, tangu mrembo huyo ambaye ni mwigizaji wa filamu kuachana na Mose Iyobo aliyezaa naye pia mtoto mmoja, lakini tofauti ya umri baina yao imekuwa gumzo mitandaoni, japo wenyewe wala hawajali.

Kwa sasa Aunt ana watoto wawili, Cookie aliyezaa na Iyobo na Heisnoma 'Nono' aliyempata na Kusah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live