Ruby; ni msanii mkali wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania ambaye wiki iliyopita alizua gumzo baada ya kusema kuwa akibahatika kufanya harusi, basi barua ya kwanza ya mwaliko katika harusi hiyo atampa aliyekuwa mpenzi wake ambapo wengi walisema si mwingine, bali ni Kusah.
Kusah na Ruby walikuwa wapenzi ambapo pia walibarikiwa kuwa na mtoto mmoja. Kusah anasema kuwa anaupokea kwa mikono miwili mwaliko huo huku akiahidi mambo mazito siku hiyo ya harusi ya Ruby.
Kwa mujibu wa Ruby, kwa sasa yupo katika uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye si msanii na hayupo tayari kumtambulisha kwenye mitandao ya kijamii.
Kusah ambaye ni mkali wa ngoma ya I Wish anasema kuwa, Ruby ana mume wake, lakini bado anazidi kumfuatilia mpaka kujua kwamba ameweka rangi gani kwenye nywele za kichwani mwake.
Kusah ambaye wiki iliyopita aliachia albam fu[pi (EP) inayokwenda kwa jina la Romantic anasema atahudhuria kwenye harusi ya Ruby huku akiahidi kumuimbia.
“Ndiyo harusi mimi nitakwenda, siwezi kukataa mwaliko, nitakwenda na nitamwimbia wimbo wangu wa I Wish, nitafurahi sana kwa sababu itakuwa ni njia mojawapo ya mwanangu kuishi maisha mazuri kwa sababu mwanamke ambaye siku zote yuko kwa mwanaume mmoja, amekaa naye maisha yanaendelea wanafanya mambo yao, ni mwanamke ambaye anajitambua.
“Kwa hiyo itamsaidia pia mwanangu kuwa na maisha mazuri kwa upande wake,” anasema Kusah ambaye mara kadhaa amekuwa akikwaruzana na Ruby anayedai kuwa jamaa huyo hahudumii mtoto.