Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kusah: Sipandi jukwaani bila milioni 5

Kusah Mn.jpeg Msanii Kusah

Sun, 15 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kusah; ni staa mpya wa Bongo Fleva ambaye amesema kwa sasa hawezi kufanya shoo yoyote ile chini ya malipo ya shilingi milioni 5.

Kusah ambaye ametisha mno na Ngoma ya I Wish anasema ingawa inategemea na aina ya shoo, lakini si chini ya shilingi milioni 5.

"Inategemea na shoo, lakini mimi pia sasa hivi sifanyi shoo chini ya milioni 5," anasema Kusah ambaye amezaa na msanii Ruby na muigizaji Aunt Ezekiel.

Kusah anasema moja ya shoo zake ghali alizofanya ambazo hawezi kuzisahau ni ile aliyofanya Nairobi nchini Kenya kwani alipata mapokezi makubwa sana kama yupo nyumbani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live