Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuondoka kwa Cheed na Killy furaha kwa waliobaki Konde Gang

Harmonize Ft Ibraah Mdomo Kuondoka kwa Cheed na Killy furaha kwa waliobaki Konde Gang

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unaweza itafsiri kauli ya staa wa muziki nchini na Mmiliki wa Record Label ya Konde Gang, Harmonize aliyoitoa kwenye moja ya post ya msanii Ibrah kama ni ya furaha kwao baada ya kuondoka kwa Cheed na Killy kwenye lebo hiyo Oktoba 10 mwaka huu.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, mwanamuziki Ibrah amepost picha ambayo imepata Comment ya Harmonize aliyeweka maneno kuwa kwa sasa wamebaki wachache hivyo ni mwendo wa ngoma baada ya ngoma.

Kuondoka kwa Cheed na Killy kunafanya Budget iliyokuwa ikiwekwa kwa wasanii hao, ihamie kwa wasanii waliobaki na kurahisisha utoaji wa kazi za wasanii husika kwenye label hiyo.

Kama Cheed na Killy walikuwa bado wapo Konde Gang na Bado CEO alikuwa akikiamsha, jiulize speed yake ya sasa itakuwaje.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live