Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuna sehemu Bongo Movie wamekosea

Kanumba+pic Kuna sehemu Bongo Movie wamekosea

Sun, 19 Jul 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By BADRU KIMWAGAWIKIENDI iliyopita ilikuwa tamu sana kwa wana Msimbazi. Ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Yanga na kuwazuia watani wao waikose tiketi ya kimataifa mwakani, kwani ilikuwa jambo kubwa kuliko hata Ubingwa wa Ligi Kuu Bara walioupata kwa msimu wa tatu mfululizo. Ndivyo Simba na Yanga zilivyo. Kama niliovyotabiri kwamba Bernard Morrison hata kuwa na maajabu ndivyo ilivyokuwa.

Jamaa aligeuka kituko, ila nikiri na kuwapa pongezi waamuzi waliolichezesha ambao awali nilikuwa nina wasiwasi nao kutokana na kutokuwa na uzoefu wa mechi za Kariakoo derby. Kama wataendelea kuchezesha walivyocheza pambano lile la Jumapili, kwa umri walionao ni wazi watafika mbali.

Kwa hakika Kariakoo derby lilikuwa pambano tamu na lililodhibitisha tofauti na mchele na chuya. Uwanja wa Taifa kuliko na tofauti kubwa ya Simba na Yanga ukiachana na zile blabla za mitaani.

Simba walikuwa bora na walistahili ushindi ule. Yanga ni kama walikuwa wamekurupushwa kwenda kwenye mchezo ule wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho.

Kama Simba wangekuwa makini wangerejea kile kipigo cha 6-0, sema ni tatizo ya wachezaji za zama hizi kuridhika na matokeo mapema. Kwa timu za wenzetu wanapopata nafasi ya kucheza na timu pinzani dhaifu wanapiga nyingi. Jumapili iliyopita Yanga ilistahili kupigwa nyingi.

Kwani ilipoteana tangu mapema kwenye mchezo huo. Bila ya shaka viongozi na wadau wa klabu hiyo ya Jangwani wamejifunza kitu kupitia kipigo hicho.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz