Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuna mchawi alivunja ndoa ya Dulla Makabila - Amina Vikoba

Makabila Sersss Kuna mchawi alivunja ndoa ya Dulla Makabila - Amina Vikoba

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Amina Vikoba ambaye ni dada wa msanii wa Muziki wa singeri nchini Dulla Makabila amesema licha ya ndoa ya mdogo wake kuvunjika yeye bado anampenda sana wifi yake na anaamini ipo siku atarudi kwenye familia yao.

Amesema Zaiylissa na Dulla walikuwa wanapendana na bado wanapendana ila tu kuna namna watu wasio wema walifanya mambo yao ya uchawi wakawatenganisha ila ana imani ipo siku watarudiana.

Kwa upande wa Zaiylissa alipoulizwa chanzo cha ndoa yake na Makabila kumomonyoka amesema mpaka sasa hajui sababu iliyovunja ndoa yake kwasababu tangu ajuane na Dulla Makabila hakuwahi kumchiti wala kumkosea na hilo hata Dulla mwenyewe analijua.

Ameongeza kuwa moja ya sababu anayoweza kuitoa japo kwa uchache huenda ni kuoana mapema bila kuchunguzana.

Yeye na Dulla Makabila walijuana Instagram na baada ya kujuana Dulla Makabila hakutaka kusubiri alimuoa haraka bila kuchunguzana tabaia kama wanaweza kwenda pamoja na matokeo yake ndoa yao iliishia kudumu kwa miezi miwili pekee huku miongoni mwa chanzo kingine cha ugomvi wao wa mara kwa mara kikiwa ni wivu uliopitiza wa Makabila.

Hata hivyo, licha ya wifi yake kumtaka arudi kwa mumewe ambaye tayari walishapeana talaka, Zaiylissa amesema kamwe hawezi kurejea kwa Makabila ingawa bado anamsumbua akimtaka arejeshe moyo nyuma warudi kama zamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live