Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Kuna mambo manne yanayomweka mjini Hamisa Mobetto

27516 Hamisa+pic Kuna mambo manne yanayomweka mjini Hamisa Mobetto

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

‘NAKUPA pole, pole umeshachelewa, pole dear Ex mwenzako nimewaiwa. Nauliza anayemmiliki ex wangu nani sasa mbona bado anapiga simu kwangu, jamani anayemmiliki ex wangu nani, oooh basi amnogeshe asipige simu kwangu’.

Hayo ni baadhi ya mashairi yaliyo kweye wimbo ‘EX wangu’ wa mwanamitindo na msanii Hamisa Mobetto aliomshirikisha Seneta Kilaka unaoendea kufanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube ukiwa umetazamwa na wafuasi 2.5 milioni ndani ya wiki mbili tu.

Mwanaspoti linakuletea mambo manne yaliyombeba mrembo huyo aliye na wafuasi zaidi ya Million 8 kwenye mtandao wake wa kijamii Instagram na kumzawadia mtaji wa mamilioni kutokana na kupata matangazo mengi.

UREMBO

Hamisa alianza kuwa maarufu Bongo mara baada ya kutwaa taji la Miss XXL, After School Bash 2010 mashindano ya urembo yaliyoandaliwa na kipindi cha XXL kutoka Clouds FM.

Hata hivyo, nyota yake ilizidi kung’ara zaidi mwaka 2011 baada ya kuibuka mshindi wa pili Miss Dar Indian Ocean na mshindi wa pili Miss Kinondoni na kuingia nusu fainali ya Miss Tanzania 2011 na Mrembo Genevieve Emmanuel ndiye aliyetwa taji kwa mwaka huo.

Kutokana kuvutiwa na fani ya urembo mwaka 2012 alishiriki mashindano ya Miss Universe Afrika na kuingia kwenye orodha ya warembo 10 bora.

MITINDO

Mrembo huyo mwenye watoto wawili aliozaa na watu maarufu akiwemo mwanamuziki Diamond Platnumz na mmiliki wa E-fm Radio, Majizzo aliamua kuanza kuchanga karata zake vizuri upande wa mitindo sehemu aliyopata mafanikio makubwa na kujenga vilivyo jina lake.

Licha ya kufanya mambo mengi ni wazi Hamisa upande wa mitindo ndipo uwezo wake unaonekana na kutambulika zaidi kuliko kwenye muziki na filamu.

Kwa miaka miwili mfululizo Hamisa alitajwa kushiriki tuzo ya Starqt Awards zinazohusisha biashara, mitindo, burudani na vitu vingine ambazo hutolewa nchini Afrika Kusini.

Mwaka 2017 alishinda kupitia kipengele cha People Choice Awards katia hafla ya utoaji wa tuzo hizo uliofanyika katika ukumbi wa Bedford View City Hall, Johannesburg nchini humo. Pia aliwania kwenye kipengele cha Super Mum ambacho hakufanikiwa kushinda.

Kabla ya hapo mwaka 2016 alishinda tuzo za Abryanz Style Fashion (ASFA2016) jijini Kampala, Uganda kipengele cha Fashionista of The Year Award East Africa.

MUZIKI

Anasema alikuwa anapenda muziki sana tangu utotoni kabla ya kuingia upande wa urembo na mitindo, lakini hakupata nafasi ya kusikika upande huo.

Kupenda kwake muziki ndiko kulimfanya kuanza kutokea kwenye video za wasanii kama video vixen na kuweza kufanya kazi na wasanii wakubwa nchini. Mwaka 2013 alionekana kwenye video ya wimbo wa Quick Rocka uitwao My Baby ambao aliwashirikisha Marehemu Mangwea pamoja na Shaa.

Kubwa zaidi ni pale alipotokea kwenye video ya wimbo wa Diamond Platnumz uitwao Salome uliotoka mwaka 2016 na kuzidi kulitangaza zaidi jina lake kwani kipindi hicho ndio alikuwa akihusihwa kutoka kimapenzi na mwanamuziki huyo mkubwa hapa nchini.

Agosti 20, 2018 Hamisa aliachia wimbo wake wa kwanza kama mwanamuziki unaokwenda kwa jina la Madam Hero ulioandikwa na msanii Foby na Prodyuza C 9.

Tayari Hamisa ameshaachia nyimbo nyingine kama Sawa, My Love, Nipoteze, Sensema aliomshirikisha Whozu na Ginger Me aliomshirikisha Singah kutokea Nigeria na sasa akitamba zaidi na kibao chake Ex.

FILAMU

Upande wa filamu Hamisa ameweza kufanya vizuri kwa kiasi chake ingawa hana mengi ya kusimulia upande huu. Baadhi ya filamu alizocheza ni pamoja na Endless Love, Vocha na Chausiku.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz