Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumpa mwanamke fedha si kuhonga, unamzawadia – Barnaba

10210 31982757 133275457536357 2578624692944371712 N TZW

Thu, 28 Jun 2018 Chanzo: bongo5.com

/>

Muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Chausiku’, akipiga stori na Wasafi TV amesema mwanaume kumpatia mwanamke fedha ni sawa na kumwagilia maua.

“Nahonga sana kaka na mpaka sasa nahonga, nawachukia wanaume wenzangu wanaosema kuhonga. Mwanamke ukimpa kitu, pesa au talanta yoyote yenye thamani haiitwi kuonga, mwanamke unamzawadia,” amesema.

“Mwanamke ni pambo ambalo linatakiwa kumwagiliwa, ukimpa mpenzi wako pesa umemwagilia ua lako, ume-protect tunda lako, mwanamke anahitaji kutunzwa, usimpomtunza mwenzako watakutunzia,” amesisitiza Barnba.

Barnaba yupo mbioni kuachia albamu yake mpya ‘Gold’ ambayo itakuwa na nyimbo zipatazo 18. Wasanii walioshiriki katika albamu hiyo ni pamoja na Juliana Kanyomozi na Jose Chameleon kutoka Uganda. Kutoka Bongo kuna Vanessa Mdee, G Nako, Ben Pol, Aslay, Barakah The Prince, Linex na Joh Makini.

Loading...
Chanzo: bongo5.com