Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Kumfananisha Mtoto Idi na Sele wa Mbosso ni kumkosea heshima'

Mbosso Sele Mj 'Kumfananisha Mtoto Idi na Sele wa Mbosso ni kumkosea heshima'

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wengi wanamfananisha Selemani na Mtoto Idi, mnakosea sana Selemani ni Mjukuu wa Idi, historia kamili hii hapa.

Miaka ya themanini Kalubandika wa bendi ya Orchestra Maquis Original, aliingia katika mahusiano na binti mmoja hivi jina limenitoka, baada ya kumpa ujauzito huyu binti Kalubandika aliukataa, bahati nzuri yule binti alipata mchumba na kuolewa hivyo hivyo na ujauzito wake.

Mwanaume aliyemuoa huyu binti anaitwa Hamidu, mtoto alipozaliwa wakampa jina la Idi. Katika wimbo wa mtoto Idi Nature anasema, Idi ni mtoto wa kwanza wa mzee Hamidu, lakini ukweli Hamidu ni baba mlezi wa Idi, baba halisi wa Idi ni Kalubandika, na ndiyo maana Idi alikuwa na tabia za Kalubandika.

Maisha yanakwenda kasi sana, Idi wa Juma Nature baada ya kukua, alimuoa kitemi mtoto wa Mama Kumbena wa Banana Zorro, wakazaa watoto watatu wote wa kiume, wa kwanza ni Side Mnyamwezi wa Mh Temba, wa pili ni Lover Boy wa Chege wa tatu ni Yahaya wa Lady Jyadee.

Katika hawa watoto watatu wa mtoto Idi wa Juma Nature, ndipo kunapatikana kizazi cha Selemani wa Mboso, Selemani ni mtoto wa Lover Boy. Kwa hiyo watu kumfananisha Selemani na Mtoto Idi ni kumkosea adabu mtoto Idi, huyu ni mjukuu wake anachokifanya sasa yeye alishakifanya miaka hiyo.

Nadhani nimeshamaliza utata.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live