Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumbe Rayvanny ndo chanzo cha Yamoto Band kufa?

Yamoto (1) Kumbe Rayvanny ndo chanzo cha Yamoto Band kufa?

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki Beka Flavour aliyewahi kuwa kundi la yamoto band lililokuwa likimilikiwa na Mkubwa Fella kwa mara ya kwanza amefunguka sababu za kundi hilo kuvinjika ikiwemo sababu ya msanii Rayvanny kupewa gari kabla yao.

“Kila mmoja alikuwa na sababu yake lakini yawezekana yeye ndiyo ilikuwa sababu yake kuu. Watu wanaweza kuona ile ni sababu ya kijinga lakini wakumbuke Aslay ameanza kufanya muziki kabla ya Yamoto Band, kitambo tu na nyimbo zake nyingi zilifanya vizuri.

“Baadaye tukaja kuungana Yamoto tukafanya ngoma nyingi, shooo kibao ndani na nje ya Tanzania. Rayvanny tulikuwa naye Mkubwa na Wanaye wakati Aslay akiwa mkubwa tu, kwa hiyo ni haki yake kulalamika na alistahili kupata gari na vitu vingine kabla hata ya Yamoto Band.

“Uongozi walikuja kumpa gari Aslay baadaye, kwa makubaliano kwamba huyu amewatangulia, tuliridhia akapewa, ulikuwa utaratibu kwamba aanze yeye na sisi tungekuja kupatiwa baadaye kama band ingekuwepo mpaka sasa, baada ya muda mchache band ikafa.

“Lakini tulikabidhiwa nyuma. Kwa watu wanaoona ni sababu ya kijinga wanakosea, mimi haikuwahi kuniumiza kwa sababu nilikuwa naishi maisha ya kawaida,” amesema Beka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live