Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumbe Rayvanny na Fahyma ilikuwa ni kiki

FAHYMAAA Rayvanny na Fahyma

Mon, 29 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rayvanny na Fahyma; ni mastaa wakubwa nchini Tanzania ambao ni wazazi wenza, lakini kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kwamba waliachana kisha wakarudiana kisha wakaachana tena.

Hata hivyo, habari mpya ni kwamba, wawili hao hawajawahi kuachana na penzi lipo palepale na hakuna mtu yeyote aliyeliharibu.

Hii stori imekuja baada ya Rayvanny kuonesha mahaba kama yote kwa Fahyma siku ya birthday ya mtoto wao wa kiume aitwaye Jaydanny.

Kabla ya hapo, mwaka jana Rayvanny alidaiwa kuwa kwenye penzi na Paula Kajala, lakini habari za ndani zinadai kuwa, hakukuwa na ukweli wowote juu ya hilo.

Inasemekana ilikuwa ni kiki tu kwa ajili ya kumnyong’onyesha Harmonize kipindi kile akiwa na uhusiano na Kajala Masanja kwa mara ya kwanza kabla hawajaachana na kuja kurudiana mara ya pili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live