Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumbe Kajala ndiye ameachwa na Harmonize?

Harmonize Kajala Ms Kumbe Kajala ndiye ameachwa na Harmonize?

Sat, 10 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chanzo cha ndani kutoka kwa wapenzi wawili ambao ni mastaa waliotikisa Bongo, Kajala Masanja na CEO wa Konde Gang, Harmonize kinadai kuwa wawili hao wameachana huku chanzo kikiwa ni Kajala.

Chanzo hicho kimepenyeza kuwa, hivi karibuni kulizuka ugomvi mzito kati ya Kajala na Harmonize huku sababu ikielezwa kuwa, siku moja Harmonize akiwa kwenye Show, alikuwa anaongea sana na mtu kwenye simu, Kajala hakupenda ile hali, akamuuliza anaongea na nani? Harmonize hakujibu!

Kuanzia hapo wakanuniana, walirudi nyumbani ugomvi ukazuka upya, Kajala akasema anaondoka kwake hakai tena kwa Harmonize.

Inaelezwa kuwa, Harmonize akavunja perfume zote za Kajala na akamwambie aondoke tu, amechoka Kumbembeleza. Kajala hakuamini kama Harmonize yupo serious hivyo akaanza kuomba Msamaha, lakini Harmonize hakumsikiliza akamfukuza kama mbwa.

Chanzo kimeenedelea kutiririka kuwa, Kajala aliamua kurudi kwake na baada ya wiki akaanza kutafuta watu wa karibu na Harmonize ili wamuombee msamaha lakini ikashindikana.

Baada ya hapo Kajala akaenda South Africa lakini akawa bado anaomba msamaha kwa Harmonize, kilichofata akapigwa Block kila sehemu kwenye mawasiliano na mitandao ya kijamii.

Hivyo juzi, ndipo Kajala akaamua kujilipua kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram ili ionekane yeye ndio amemuacha Harmonize, ila ukweli ni kwamba yeye ndio ameachwa.

Aidha, inaelezwa kuwa Harmonize ameonekana katika vunga vya Tegeta akiwa na moja ya Range alizomnunulia Kajala ikiwa imetolewa lile jina la Kajala 1, na haina kabisa Plate Number.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live