Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kukamatwa kwa mshukiwa wa mauaji ya 2Pac, dada afunguka

Tupac Sister Hollywood Tupac Shakur na dada yake

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dada wa aliyekuwa Msanii Maarufu marehemu Tupac Shakur, amesema kukamatwa kwa Kiongozi wa genge anayehusishwa na mauaji ya Tupac ni ”tukio na wakati muhimu”.

Kupitia mtandao wa Instagram Bi. Sekyiwa Shakur ameandika ujumbe uliosema ”leo ni siku ya ushindi” lakini ”hukumu iliyohifadhiwa” hadi hatua za kisheria zitakapokamilika.

”Ni muhimu kwangu kwa dunia, nchi ,mfumo wa haki na watu wetu kukiri kifo cha mtu huyu, kaka yangu, kijana wa mama yangu, kijana wa baba yangu”

”Kumekuwa na mikono mingi iliyohusika na kuna mengi yanayozunguka maisha na kifo cha kaka yangu Tupac na familia yetu ya Shakur kwa ujumla. Tunatafuta haki katika pande zote” alisema Sekyiwa.

Akizungumza na Shirika la habari la CNN Mopreme Shakur ambaye ni kaka wa marehemu, amesema “kushtakiwa kwa Duane ni kuchungu na kutamu, tumepitia miaka mingi ya maumivu, walikuwa wanafahamu kuhusu huyu mtu ambaye amekuwa akiongea tu kwa miaka mingi”

”Kwahiyo kwanini sasahivi? kwetu hii bado haijaisha, tunataka kujua kwanini na kama kulikuwa na washirika wengine”.

Ijumaa iliyopita Polisi wa Nevada walimshtaki Duane ”Keffe D” Davis (60) kwa kosa la mauaji kwa kutumia silaha ya moto.

Tupac ambaye alikuwa nyota wa mziki wa Hip Hop aliuawa mwaka 1996 kwa shambulio la risasi huko Las Vegas.

Kwa mujibu wa Polisi, Duane alipanga na kuamuru kufanyika kwa shambulio hilo baada ya mpwa wake kupigana na Tupac wakiwa Casino.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live