Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuizuia nyota ya Zuchu kung'ara haiwezekani

Zuchu Gauni Kuizuia nyota ya Zuchu kung'ara haiwezekani

Thu, 4 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuizuia nyota ya Zuchu ni sawa na kuziba mwanga kwa kiganja cha mkono. Mwimbaji huyo wa Bongofleva kutoka WCB Wasafi, ameweka historia ya kuwa msanii wa kike katika nchi zilizopo chini ya Jangwa la Sahara barani Afrika kuwa na subscribers wengi katika mtandao wa YouTube.

Zuchu ambaye alitoka kimuziki miaka miwili iliyopita, amefikisha subscribers Millioni 2.1, nafasi ambayo amempiku msanii toka Nigeria, Yemi Alade mwenye subscribers Millioni 2 ambaye alikuwa anashikilia. Kwa sasa nafasi hiyo inashikiliwa na Zuchu.

Kweye top 10 ya orodha hiyo, nafasi ya kwanza ni Zuchu, kisha anafuata Yemi Alade huku nafasi ya sita ikishikiliwa na Mtanzania, mwimbaji Nandy akiwa na subscribers Millioni 1.7.

Zuchu ame-share rekodi yake hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ametoa pia pongezi kwa wanawake wengine kuwepo kwenye orodha hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live