Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuingia usiku wa Zuchu Sh5 milioni

Zuchu+pic Zuchu msanii mpya WCB

Thu, 16 Jul 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Nasra AbdallahUongozi wa WCB umeanika kiingilio ambacho watu watapaswa kulipa kuingia katika usiku wa shukrani wa msanii Zuchu.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Julai 13, 2020 na Mkurugenzi wa lebo ya WCB, Diamond Platnumz alipokuwa akiongelea onyesho la msanii huyo  litakalofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Diamond amesema onyesho hilo wanataka kulifanya la hadhi ya juu ambapo pia viingilio vimetofautiana kulingana na mahitaji ya watu.

Amesema kiingilio cha chini kitakuwa ni Sh 50,000, kikikufatiwa na Sh100,00 Sh1 milioni, milioni, Sh3 milioni na Sh5 milioni.

"Kuna watu wenye hela zao watataka kuingia VIP nasi hatujawasahau katika hili kwa kuwa tunataka kulifanya onyesho la hadhi,na tuna imani hawatajutia watakaokuja," amesema.

Kwa upande wake Zuchu amesema katika nusu ya mapato yatakayopatikana ameomba yaende kwa wasichana wenye uhitaji.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz