Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuhusu Project ya Upo Hapo, Tutegemee kundi jipya kutoka kwa Mwana FA, AY na Fid Q? Majibu yako hapa.

1046 Screen Shot 2018 01 03 At 3.12.59 PM 660x400.png TZW

Thu, 4 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Yawezekana wewe ni miongoni mwa watu waliovutiwa na ujio wa wimbo wa Mwana FA, AY na Fid Q unaoitwa Upo Hapo na ndoto au mipango yako ulikua unatamani kuwaona wakiwa kundi kama ilivyo kwa baadhi ya makundi ya muziki hapa Tanzania kwa mifano kama kundi la Roma na Stamina(Rostam), Weusi na mengine mengi.

Kupitia Clouds FM kwenye kipindi cha XXL, Mwana FA kaliweka wazi hilo kwa kusema >>‘Tunaweza kufanya kazi kwa pamoja yaani watu wengi yaani tukakusanyika tukawa tunafanya kazi yaani watu wawili,watatu au wanne lakini kutengeneza group kwa uchumi wa muziki ulivyo sasa hivi ni kazi ngumu kidogo’

‘Tunaweza kufanya Group ya Project labda tunataka kufanya kazi hii tukaifanya mwanzo hadi mwisho ikimalizika kila mtu anashika 50 zake, hakuna uwezekani wa kutengeneza group halafu ikawa inafanya kama group moja kwa moja muziki wa group ulishashindwa’ – Mwana FA.

Mwana Fa aliwahi kusema kuhusiana na kuacha muziki, Ulimsikia? Bonyeza play kumtazama.

Chanzo: millardayo.com