Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kufuru! Diamond amnunulia mama yake saa ya Tsh mil 53.2

Diamond Mama D Diamond amnunulia mama yake saa ya Tsh mil 53.2

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CEO wa Levo ya WCB na supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amemnunulia mama yake, Bi. Sandra maarufu kama ‘Mama Dangote’ saa ya thamani aina ya Hublot Geneve.

Saa aina ya Hublot Geneve inakadiriwa kuuzwa Dola 22,700, wastani wa Sh53.2 milioni.

Siku ya Ijumaa, Mama Dangote alionyesha saa maridadi aina ya Hublot Geneve kwenye mkono wake na kufichua kuwa mwanawe alimnunulia.

“Mtoto wangu,” aliandika chini ya video hiyo.

Utakumbuka mapema wiki hii, Bosi huyo wa WCB Wasafi alionyesha mapenzi makubwa kwa msanii wake Zuchu kwa kumnunulia pambo la bei ghali.

Staa huyo ambaye kwa sasa yuko Uingereza alionekana kwenye video akiwa ameshika cheni maridadi ya fedha yenye kichwa cha malkia ambayo alinunua katika duka moja la mapambo jijini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live