Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Kuanzia November 8, Hakuna kuingia Marekani kama haujachanja

Screenshot 2021 10 17 At 13.35.55 660x400.png Kuanzia November 8, Hakuna kuingia Marekani kama haujachanja

Sun, 17 Oct 2021 Chanzo: millardayo.com

Moja ya habari kubwa za wiki hii ni huu uamuzi wa Marekani kutangaza kwamba itaanza kuwaruhusu Abiria wa kimataifa waliochanjwa chanjo kamili ya COVID-19 tu.

Naibu Afisa wa Habari katika Ikuku ya White House Kevin Munoz ametangaza hilo kupitia ukurasa wa Twitter na kuongeza kuwa sera hiyo itaongozwa na uzingatiaji wa afya ya umma na masharti yaliyopo mara kwa mara.

March 2021 mwaka uliopita Marekani ilifunga mipaka na kuwazuia Wasafiri kutoka mataifa mengine ikiwemo Umoja wa Ulaya, China, Uingereza, India na Brazil kama juhudi za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona na sasa chini ya sera mpya iliyoainishwa mwezi uliopita Wasafiri ambao wamepata chanjo watahitaji kupimwa kama kawaida siku tatu kabla ya kusafiri kwenda Marekani.

Chanzo: millardayo.com