Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Krystyna Pyszkován Miss World mpya amewahi kufundisha Tanzania

Miss A0013 Krystyna Pyszkován

Sun, 10 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni ukweli usiopingika kwamba kuanzia jana March 9 dunia imeanza kumzingatia Krystyna Pyszkován kwa uzito mkubwa kuliko ilivyokua hapo awali na hii ni baada ya Malkia huyo wa nguvu kutangazwa kuwa Miss World 2024 huko Mumbai, India katika shindano ambalo limehusisha Warembo 112 kutoka Nchi mbalimbali.

Sote tunafahamu kwamba unapofika muda wa kipengele cha Beauty with purpose, Warembo wanaolisaka taji hilo huonesha ‘project’ walizozifanya kugusa Jamii mbalimbali ambapo hapo ndipo akatusanua kwa kuonesha sehemu ya project yake hiyo ya Arusha, Tanzania miaka mitatu iliyopita (mwaka 2020).

Kwenye video ya dakika 7, Krystyna baada ya kukuta baadhi ya Watoto katika mazingira magumu Kijijini wakishindwa kwenda Shule ili kusaidia Wazazi na kutafuta pesa ya kula.

Krystyna Pyszkován (24) ambaye ameshinda taji la Miss World 2024 jana March 09, 2024, moja ya vitu vilivyompa ushindi ni story yake ya Beauty with purpose ambayo ameitengenezea makala ya kusisimua iliyoanzia Nchini Tanzania akielezea jinsi alivyofanikisha kuanzishwa kwa Shule moja Jijini Arusha kwa kushirikiana na Sonta Foundation.

Wao kama Sonta Foundation waliamua kuanza ujenzi wa Shule itakayosaidia kutoa elimu bora kwa lugha ya Kiingereza kwa Watoto zaidi ya 320 huku wakipikiwa chakula shuleni na kuwapa maji safi na salama waliyoyachimba kwenye visima na kuyapandisha kwenye matenki kisha yanasambazwa kwenye mabomba Shuleni hapo na moja ya vitu vya kufurahisha zaidi ni kwamba Krystyna ameingia darasani yeye mwenyewe na kujitolea kufundisha Watoto hao mara kadhaa akiwa nchini Tanzania.

“Tuliamua kuanzisha mpango wa kuruhusu Watu kutoka Mataifa mbalimbali kuja kufundisha na mimi ni mmoja wao niliyejitolea kuingia darasani mwenyewe na kufundisha, tunatoa pia chakula cha mchana kwa Wanafunzi 320 kila siku shuleni.

"Baadhi ya Wanafunzi kabla ya program hii walikua wakikaa shule kwa saa nane bila kula kutokana na hali duni za Wazazi wao lakini toka January 2023 Wanafunzi wamekua wakipata chakula cha mchana kila siku na tumeona matokeo mazuri darasani, mahudhurio na hata afya zao, ” amesema Krystyna.

Krystyna ni Mwanafunzi kwenye degree mbili kwenye Sheria na Utawala kwenye biashara na pia ni Mwanamitindo wa Kimataifa mwenye urefu wa 180 CM akiwa anaweza kuongea lugha ya Kiingereza, Kipolish, Kislovakia na Kijerumani, ni Mwazilishi wa Krystyna Psyzko Foundation na pia anapenda muziki na sanaa akiwa ametumia miaka tisa kwenye Academy ya sanaa na ni fundi mzuri wa kupiga violin

Chanzo: www.tanzaniaweb.live