Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kris Jenner afunguka kuvujisha video ya ngono ya mwanaye Kim Kardashian

Kris Jenner.jpeg Kris Jenner afunguka kuvujisha video ya ngono ya mwanaye Kim Kardashian

Mon, 12 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

The Late Late show na James Corden, Alhamisi iliyopita, Mama mzazi wa watoto 6 maarufu na drama nyingi (The Kardashians Family), Kris Jenner (66) amefunguka mengi kuhusu familia yake alipowekwa kwenye kiti cha kugundua uongo (The Lie Detector Machine).

Miongoni mwa vitu alivyoulizwa mama huyo ni kutaja mtoto wake pendwa zaidi kati ya watoto wake 6 (Kourtney Kardashian, Kim Kardashian, Khloé Kardashian, Rob Kardashian, Kendall Jenner na Kylie Jenner), na kama ni kweli alihusika kuvujisha mkanda wa ngono wa mwanaye Kim Kardashian mwaka 2007.

Kris Jenner amemtaja last born wake Kylie Jenner (25) kama ndiye mtoto wake pendwa zaidi, lakini akakanusha kuhusika kuvujisha mkanda wa ngono (connection) wa Kim Kardashian kama ilivyo daiwa na mwanamuziki na muigizaji Ray J, aliyekuwa mpenzi wa Kim Kardashian kwa wakati huo ambaye pia ni muhusika kwenye connection hiyo.

Mwezi May mwaka huu, Ray J alidai hakuwahi vujisha sexy tape yake na Kim, na hayakuwa makubaliano yao, akiiambia Daily Mail, Ray J alidai Kim alimpatia mama yake mkanda wao wa ngono ambapo baadae, Kris Jenner akauvujisha.

Tape hiyo ilivuja mwaka 2007 na huo ndio ukawa mwanzo wa umaarufu wa Kim Kardashian hadi leo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live