Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kontawa afunguka mpango wake wa kwenda jeshini

Kontawa Afunguka Mpango Wake Wa Kwenda Jeshini Kontawa afunguka mpango wake wa kwenda jeshini

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: Mwananchi

Mwanamuziki wa hip-hop nchini Kontawa wakati akizungumza na Mwananchiscoop ameeleza mpango wake wa kwenda jeshini ulipofikia.

Mwezi Agosti msanii huyo aliomba kuingia jeshini kwenye mafunzo ya kujitolea ya miezi sita, na kutokana na ombi hilo ameiambia @mwananchiscoop kuwa maombi yake anafikiri yamesikilizwa na siku siyo nyingi watu wataona kile ambacho aliomba kukifanya.

Kontawa hakuishia hapo akasema watu wategemee kuona mwanajeshi msanii kwa sababu hata yeye ana hamu ya kwenda jeshini.

Msanii huyo alitoa ombi hilo wakati akikabidhi nguo yake yenye kufanana na sare za jeshi, kutokana na agizo lililokuwa limetolewa na JWTZ kwa watu wenye nguo za kufanana na sare hizo kuzikabidhi kwa jeshini.

Chanzo: Mwananchi