Mwanadada Nayce Moshi ambaye ni kondakta wa Mabasi ya Kampuni Fulani zinazofanya safari yake kutoka Dar es salaam kwenda Arusha, ameamua kuweka wazi kuhusiana na maisha yake baada ya watu kumwita yeye ni staa.
"Sipendi kuitwa Staa kwasababu sipendi maisha ya Kistaa yana gharama, yatanifanya niishi maisha ya kujificha na ya kumulikwa na camera kila mahali. Naomba watu wanichukulie wa kawaida tu kwasababu bado nina safari ndefu kwenye mapambano ya maisha yangu, nina ndoto nyingi ambazo natamani kuzitimiza"
"Kuhusu bei ya kunyoa kwangu na suti ninayovaa naona watu wengi hawakuamini waliona kama ni vitu vya bei kubwa sana tofauti na kazi ninayoifanya ya ukondakta. Mimi mbali na kuwa konda pia nina kazi nyingine.
"Nina mikataba na makampuni mbalimbali nawatangazia biashara, nafanya kazi usiku na mchana kuna siku nalala saa nane usiku naamka saa tisa, kuna siku nalala nusu saa tu kwa siku nzima, natafuta pesa yangu kwa shinda siwezi kuitumia kwa shida lazima nipendeze muda wote," amesema Nayce Moshi,