Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kolabo ya Kiba, Harmonize Yatabiriwa

Alikiba Harmonize Kolabo ya Kiba, Harmonize Yatabiriwa

Sat, 5 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BAADA ya Mfalme wa Bongo Fleva, King Kiba na Harmonize kuoneka kama wana ukaribu f’lani, mtangazaji na mwigizaji Mwijaku ametabiri uwepo wa kolabo ya wawili hao ndani ya mwaka huu.

Mwijaku amefichua ishu hiyo wakati akizungumzia orodha ya wasanii 21 Bora Tanzania ambayo imetolewa na Taasisi ya Haki Miliki Tanzania (COSOTA) kisha kuibua mjadala kama wote.

Orodha hiyo imemuorodhesha Diamond Platnumz akiwa namba tano huku Kiba akiibuka namba moja na Harmonize akiwa namba nne.

“Hivi karibuni na niliwaambia, inakuja kolabo, Kiba pamoja na Harmonize, mimi nipo kwenye mipango, mashabiki kaeni mkao wa kula,” anasema Mwijaku.

Harmonize au Harmo akiwa kwenye Lebo ya Wasafi hapakuwepo uhusiano wa karibu baina yake na King Kiba, lakini tangu aondoke wamekuwa karibu.

Jumatatu Harmonize aliposti wimbo wa King Kiba kwenye Insta Story yake kuonesha ukaribu baina ya wasanii hao wawili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live