Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Koffi kuwaburudisha Wanasimba

98206 Pic+kofii Koffi kuwaburudisha Wanasimba

Fri, 6 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

NGULI wa muziki wa dansi kutoka DR Congo, Koffi Olomide leo Ijumaa usiku atajumuika na wanachama wa klabu ya Simba wakati wa uzinduzi wa matumizi wa kadi mpya za wanachama wao. Koffi yupo nchini ambapo kesho Jumamosi atakuwa na shoo yake jijini hapa lakini kabla ya shoo hiyo atawaburudisha wanachama hao ambao kesho kutwa wao watakuwa uwanjani kuishangilia timu yao itakapovaana na Yanga mechi ya Ligi Kuu. Mechi hiyo ambayo ni ya mzunguko wa pili wa ligi itachezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba wameweka taarifa hiyo kwenye ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa Facebook na kutangaza kuwa halfa hiyo itaanza saa 12:00 jioni mpaka saa 2:00 usiku katika hoteli ya kitalii iliyopo katikati ya Jiji. Wanachama wa Simba hivi sasa wanatumia kadi mpya za uanachama ambazo ni za kielektroni tofauti na hapo awali.

Chanzo: mwananchi.co.tz